Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Mheshimiwa Mbarouk Nassor Mbarouk, tarehe 02/03/2014 aliwasilisha Hati za Utambulisho kwa Mtukufu Sheikh Mohammed bin Rashid Al Makhtoum, Makamu wa Rais UAE, Waziri Mkuu na Mtawala wa Dubai, jijini Abu Dhabi, UAE. Sherehe hizo zilizofanyika kwenye Kasri ya Al Mushrif, zilihudhuriwa na viongozi mbali mbali wa Kitaifa wa UAE.
Mheshimiwa Balozi akiwasilisha salaam kutoka kwa Mheshimiwa Rais wa Tanzania na kujitambulisha rasmi.
Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akiwasilisha Hati za Utambulisho kwa Mtukufu Sheikh Mohammed bin Rashid Al Makhtoum, Makamo wa Rais wa UAE, Waziri Mkuu na Mtawala wa Dubai, kwenye kasri ya Al Mushrif, mjini Abu Dhabi, UAE.
