Mheshimiwa Lt. Jen. (Mst), Yacoub Hassan Mohammed, Balozi wa Tanzania, Abu Dhabi, nchini Umoja wa Falme za Kiarabu (U.A.E) amewakaribisha na kuwapa semina juu ya kazi za Ubalozi, majukumu ya Ofisi ya Ubalozi na Ofisi ya Konseli Kuu, uhusiano kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Umoja wa Falme za Kiarabu (U.A.E) kwa wanafunzi 500 waliotembelea Ubalozi wa Tanzania hapa Abu Dhabi.
Wanafunzi hao 500 kwa awamu tatu walipokelewa na Mheshimiwa Lt. Jen. (Mst), Yacoub Hassan Mohammed, Balozi wa Tanzania, Abu Dhabi, nchini U.A.E. na Bw. Mohamed Kamal Mohamed, Kaimu Konseli Mkuu, Konseli Kuu ya Tanzania iliyopo Dubai.
Uratibu wa Ziara hii ya kimafunzo umeratibiwa na Global Education Link kampuni kutoka Tanzania kwa kushirikiana.
